Archive | November 2011

PIGO JINGINE KATIKA UTAFITI DHIDI YA VVU

Wataalamu wetu wa VOICE study iliyokuwa inatafiti  Mafuta ya Kupaka Ukeni ya Tenofovir  wamelazimika kusitisha matumizi ya dawa hiyo katika uutafiti kwa kushindwa kuzuia Maambukizi ya VVU. Hii ni setback nyingine katika utafiti kwani awali kulikuwa na matumaini makubwa sana ya Mafanikio. Tafiti zinaonesha kuwa Tenofovir Rectal gel inaonesha mafanikio kutokana na muundo tofauti wa seli katika kingo za unyuma wa mwanaume na uke. Hata hivyo kwa kuwa Gates Foundation bado imeweka mabilioni ya fedha tunatarajia watafiti wetu haatakatishwa tamaa na mafanikio hasi haya.

SOMA HAPA: http://www.niaid.nih.gov/news/newsreleases/2011/Pages/VOICEdiscontinued.aspx

Karibu katika Marafiki wa Maisha

Marafiki wa Maisha ni sehemu ambayo utapata Habari mpya za Elimu na Mafunzo ya Afya, Ushauri wa Kiafya  na Taarifa za Tafiti mpya za Afya. Lengo letu ni kuwawezesha Wananchi kuwa na uwezo wa kuepuka Magonjwa yanayoepukika ili Kuboresha Afya na Maisha yao.     

 Tunao Wataalamu waliobobea Kimataifa katika kutoa huduma Zifuatazo:

  • Kuendesha Mafunzo ya Afya na Ushauri

  • Kuandaa Machapisho na Majarida ya Afya

  • Kuandika mapendekezo ya Miradi na Tafiti za Afya

  • Kusimamia Utekelezaji wa Miradi na Tafiti za Afya

  • Kuandika Ripoti za Miradi na tafiti za Afya

  • Kufanya kaguzi za Utekelezazi na Mafanikio ya miradi ya Afya

WASILIANA  NASI